• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Cristiano Ronaldo aondoka kiwanjani kabla ya kipenga cha mwisho

  (GMT+08:00) 2019-11-12 09:11:11

  Cristiano Ronaldo ameripotiwa kuondoka kwenye Uwanja wa Allianz kabla ya kipenga cha mwisho kwenye mechi ambayo Juventus ilijipatia ushindi mwembaba wa 1-0 dhidi AC Milan ya Serie A iliyochezwa Jumapili, baada ya kubadilishwa katika mechi ya pili kwa wiki. Paulo Dybala alichukua nafasi ya Ronaldo katika dakika ya 55 na mshambuliaji huyo wa Argentina akaingia na kufunga bao la ushindi baada ya dakika 22 na kuiweka Juventus kileleni mwa Serie A mbele ya Inter Milan. Ronaldo ambaye ni mshindi Ballon d'Or mara tano alionekana kukasirika wakati anatoka na kumtupia maneno kocha Maurizio Sarri kabla ya kuelekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na kwa mujibu wa Sky Sport Italia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 aliondoka kwenye uwanja huo dakika tatu kabla ya mechi kumalizika. Hata hivyo Sarri alisema yeye hajui kama Ronaldo aliondoka kwenye uwanja mapema au la.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako