• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • RIADHA: Kipkorir anyakua ubingwa wa Athens Marathon

  (GMT+08:00) 2019-11-12 09:11:53

  John Komen Kipkorir aliendeleza ubabe wa Kenya katika mbio za kilomita 42 za Athens nchini Ugiriki baada ya kunyakua taji la mwaka 2019 kwa saa 2:16:34. Katika mbio hizi zilizokimbiwa katika mvua na maeneo ya milima, Komen, mwenye miaka 42, alimpita Felicien Muhitira kutoka Rwanda zikisalia mita 600 na kutwaa taji. Ushindi huu wa Athens Marathon kwa Kenya ni wa 16 tangu mwaka 2001. Ni mwaka wa nne mfululizo mwanamume kutoka Kenya kutwaa taji la Athens Marathon baada ya Luka Rotich (2016), Samuel Kalalei (2017) na Brimin Kipkorir (2018). Hapo Jumapili, Muhitira, mwenye miaka 25, aliridhika katika nafasi ya pili kwa kukimbia kwa saa 2:16:43 naye Mgiriki Konstantinos Gkelaouzos (2:19:02) akafunga mduara wa tatu-bora. Eleftheria Petroulaki alishinda taji la wanawake kwa saa kutumia saa 2:39:00. Mkenya Shelmith Nyawira alikuwa ameshinda taji hili mwaka 2018. Washiriki 60,000 kutoka zaidi ya mataifa 100 walihudhuria makala haya ya 37 wakiwemo 20,041 katika mbio za kilomita 42.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako