• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • TENISI: Rafael Nadal ashindwa na Alexander Zverev kwenye ATP Finals

  (GMT+08:00) 2019-11-12 09:12:13

  Kampeni za Rafael Nadal za kukamilisha mwaka akiwa mcheza tenisi namba moja duniani zimeingia dosari baada ya kushindwa na bingwa mtetezi Alexander Zverev kwenye ATP Finals. Mhispania huyo ambaye hali yake kiafya iliingia matatani kabla ya mechi za kumaliza msimu huko London baada ya kupata majeraha mgongoni, alishindwa kwa 6-2 6-4 katika mechi ya ufunguzi hatua ya raundi robin. Nadal, alionekana hakuwa sawa kwenye mchezo huo na kufanya makosa kadhaa. Awali Stefanos Tsitsipas alimshinda mwanagenzi mwenzake Daniil Medvedev. Mgiriki huyo mwenye miaka 21 alimgaragaraza Mrussia kwa 7-6 (7-5) 6-4 katika O2 Arena. Novak Djokovic, ambaye anaweza kumpiku Nadal nafasi yake ya kwanza duniani wiki hii, ameongoza kundi jingine baada ya kushinda Jumapili. Wachezaji wawili vinara katika kila kundi baada ya hatua ya raundi ya robin watasonga mbele kwenye nusu fainali siku ya Jumamosi. Michuano hiyo ya kumalizia msimu ya wanaume inayofanyika London inashirikisha wachezaji bora wanane wa mwaka.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako