• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika wazitaka pande husika za Sudan Kusini kutekeleza haraka ahadi za makubaliano yaliyofikiwa hivi karibuni

    (GMT+08:00) 2019-11-12 10:25:59

    Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Faki Mahamat amezitaka pande za Sudan Kusini zinazopigana kutekeleza haraka ahadi kuu za makubaliano yaliyofikiwa hivi karibuni.

    Bw. Mahamat amesema hayo akikutana na kiongozi wa upinzani wa Sudan Kusini Bw. Riek Machar katika makao makuu ya Umoja huo huko Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia.

    Baada ya kukutana na kiongozi huyo, Bw. Mahamat amesema yeye na kamishna wa Umoja wa Afrika anayeshughulikia amani na usalama Bw. Smail Chergui, walimpokea Dkt Riek Machar aliyewajulisha maendeleo baada ya mkutano wa kilele wa pande tatu kuhusu makubaliano ya utatuzi wa mapigano nchini Sudan Kusini.

    Mara baada ya kukutana na Bw. Machar, Bw. Mahamat ametoa taarifa kupitia mitandao ya kijamii akizitaka pande zote kutekeleza haraka makubaliano kama walivyoahidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako