• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • WHO yasema eneo la Afrika kusini mwa Sahara haliko katika njia ya kutimiza malengo ya maendeleo endelevu ya afya

  (GMT+08:00) 2019-11-12 10:26:14

  Shirika la Afya la Dunia WHO limesema, nchi za Afrika Kusini mwa Sahara haziko katika njia ya kutimiza malengo ya maendeleo endelevu kuhusu kupunguza kiwango cha vifo vya wajawazito na watoto wachanga.

  Mkurugenzi wa idara ya afya za wajawazito, watoto wachanga, watoto na vijana ya shirika hilo Bw. Anshu Banerjee, amesema huko Nairobi kuwa malengo ya maendeleo endelevu ni makubwa, hivyo yanahitaji uwekezaji mkubwa na endelevu ili kuyatimiza.

  Amesema hayo katika mkutano wa 24 ya bodi ya wakurugenzi wa uhusiano wa kiwenzi kwa wajawazito, watoto wachanga na watoto, huku akiongeza kuwa tangu mwaka 2015, kiwango cha vifo vya wajawazito na watoto wachanga kinapungua, lakini kupungua huko ni polepole, na kutokana na kasi ya sasa ya maendeleo, eneo la Afrika kusini mwa Sahara halitaweza kutimiza malengo hayo .

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako