• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Naibu waziri mkuu wa China akutana na wajumbe wa timu za madaktari wa China walioko Afrika

  (GMT+08:00) 2019-11-12 18:40:06

  Naibu waziri mkuu wa China Bibi Sun Chunlan ambaye hivi sasa yuko ziarani Ghana, amekutana na wajumbe wa timu za madaktari wa China walioko katika nchi 17 za Afrika na kuzungumza nao.

  Bibi Sun amesema, kwa muda mrefu, madaktari hao wamekumbana na kutatua matatizo magumu na kusifiwa na nchi zinazopokea misaada na jumuiya ya kiamtaifa, na kusema misaada ya matibabu ya China kwa Afrika ni mfano mzuri wa uhusiano kati ya China na dunia.

  Bibi Sun pia amesistiza kuwa, wahudumu hao wa afya wanapaswa kuendelea kutia nguvu kuboresha viwango vya afya katika nchi husika, kuvumbua mfumo wa kutoa misaada, kusukuma mbele maendeleo ya afya ya nchi hizo, na kuongeza uaminifu na mawasiliano ili kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa kwenye Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika na kuhimiza ustawi na maendeleo ya pamoja ya dunia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako