• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema kusimamisha vurugu na kurudia utaratibu ni jambo muhimu zaidi kwa mkoa wa Hong Kong

    (GMT+08:00) 2019-11-12 18:41:22

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, serikali kuu ya China inaunga mkono serikali na polisi ya mkoa wa utawala maalum wa Hong Kong kutekeleza sheria ili kulinda utaratibu wa jamii na usalama wa raia.

    Bw. Geng amesema, hakuna nchi inayoruhusu mtu kunyang'anya silaha askari polisi, wala kushambulia na kutishia usalama wa polisi, na kuongeza kuwa kitendo hicho kitadhibitiwa ipasavyo.

    Bw. Geng pia amesisitiza kuwa, kusimamisha vurugu na kurudisha utaratibu ni jambo muhimu zaidi kwa Hong Kong, pia ni wito kwa sekta mbalimbali mkoani humo. Amesema mambo ya Hong Kong ni mambo ya ndani ya China, na nchi yoyote ya nje hairuhusiwi kuingilia kati mambo hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako