• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Sterling afukuzwa kambini kwa utovu wa nidhamu

  (GMT+08:00) 2019-11-12 18:46:47
  Mchezaji wa timu ya taifa ya Uingereza na klabu ya Manchester City Raheem Sterling ameondolewa katika Kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kinachojiandaa dhidi ya Montenegro katika kufuzu michuano ya Euro 2020 kwa kosa la ugomvi. Kocha wa timu ya Taifa ya Uingereza Gareth Southgate amefafanua kuwa wamelazimika kuchukua uamuzi huo baada ya kuzuka ugomvi baina ya Raheem Sterling na Joe Gomes katika uwanja wa mazoezi wa St. George's Park. Sterling wa Manchester City, alitunishiana kifua na beki wa Liverpool, Joe Gomez, wakati wa ushindi wa Liverpool 3-1 huko Anfield Jumapili iliyopita.
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako