• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • RAGA: Kabras Sugar wasalia mbele Kenya Cup kwa alama 15 zaidi

  (GMT+08:00) 2019-11-12 18:47:06
  Wafalme wa mwaka 2016 Kabras Sugar na mabingwa watetezi KCB wako bega kwa bega katika msimamo wa Ligi Kuu ya Raga (Kenya Cup) ya msimu 2019-2020 kwa alama 15, baada ya kuandikisha ushindi wa tatu mfululizo wikendi. Wanasukari wa Kabras wanashikilia nafasi ya kwanza kwa ubora wa alama baada ya kuwafunga mabingwa wa zamani Impala Saracens kwa alama 27-3 katika mechi iliyochezwa uwanja wa Kakamega Showground. Wanabenki wa KCB, ambao wanafukuzia taji la nne mfululizo, nao waliwaliza washindi wa mwaka 2013 na 2014 Nakuru kwa alama 50-13, uwanjani Ruaraka na kurukia nafasi ya pili kutoka nambari tatu. KCB ilinufaika kupiga hatua moja mbele pale Impala iliyoshikilia nafasi ya pili ilipopoteza mechi dhidi ya Kabras na kupoteza alama muhimu. Homeboyz nayo ilifaidika na masaibu ya Impala ikiimarika kutoka nafasi ya tano hadi nambari tatu baada ya kuichapa Menengai Oilers 25-20 uwanjani Jamhuri. Homeboyz, Kabras na KCB ni klabu ambazo hazijapoteza mchuano msimu huu.
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako