• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Maelfu ya Waganda wahudhuria mafunzo ya kujenga uwezo nchini China

  (GMT+08:00) 2019-11-12 19:56:37

  Wataalam takriban 4,400 wa Uganda pamoja na wabunge na watumishi wa serikali wamehudhuria mafunzo ya muda mfupi ya kujijengea uwezo yaliyotolewa nchini China.

  Akizumza kwenye hafla ya kuwapokea wanafunzi iliyofanyika katika Wizara ya Biashara ya China, naibu mkurugenzi wa Chuo cha Kimataifa cha Biashara kwa Maofisa, Lei Hao amesema, Zaidi ya Waganda 600 walihudhuria mafunzo ya aina mbalimbali ikiwemo utawala, sera za umma, elimu, uchumi na kilimo.

  Naye kamishna wa maendeleo ya sera na ujenzi wa uwezo katika ofisi ya rais wa Uganda Bw. Abubakar Muhammad Moki amesema, mafunzo ni muhimu katika kusaidia maendeleo ya kasi ya Uganda, pia amesema ni muhimu kwa washiriki wa mafunzo hayo kutekeleza kile wanachojifunza.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako