• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika yapata mafanikio katika kuondoa visa

    (GMT+08:00) 2019-11-12 19:57:01

    Kiashiria cha Uwazi wa Visa Afrika kwa mwaka 2019 kimeonyesha kuwa bara hilo limepata mafanikio makubwa katika kuondoa visa kwa kuwa Waafrika wanaweza kusafiri kwenye nchi zaidi bila ya kuhitaji visa.

    Ripoti iliyoandaliwa na Kamisheni ya Umoja wa Afrika na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imesema, kwa mara ya kwanza, Waafrika wanaweza kuingia kwenye nchi karibu 27 za bara hilo bila ya kuhitaji visa, ama kupata visa wanapofika.

    Mchakato wa kuondoa visa barani Afrika unafuatia kasi inayoendelea ya maingiliano zaidi kati ya nchi za bara hilo, na inaashiria kuwa wabunge wa nchi za Afrika wanachochea mageuzi, na kuwafanyia urahisi wafanyaiashara wa bara hilo, wawekezaji, wanafunzi na watalii kusafiri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako