• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Mkenya Mwingine afungiwa kwa kutumia dawa za kusisimua misuli

    (GMT+08:00) 2019-11-13 08:11:59

    Mahakama ya Nidhamu za Wanariadha jana imesema kuwa mkimbiaji aliyekuwa akishika rikodi ya dunia ya nusu marathon Mkenya Abraham Kiptum amepigwa marufuku kwa miaka minne kwenye riadha kwa kujihusisha na matumizi ya dawa za kusisimua misuli. Marufuku hiyo imefuatia hitilafu zilizojitokeza kwenye vipimo vya Kiptum vilivyotumika kuangalia kama anatumia dawa hizo. Kupitia mtandao wake wa Twitter mahakama hiyo imetoa taarifa ikisema imemfungia mwanariadha huyo wa mbio ndefu kwa miaka mine hukumu ambayo ilianzia Aprili 28 mwaka huu. Mahakama ilishuku Kiptum mwenye miaka 30 kwamba damu yake ina dawa za kusisimua misuli, lakini mkimbiaji huyo alikataa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako