• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Jeraha lamfanya Mohamed Salah kukosa michuano ya kufuzu kombe la Mataifa ya Afrika AFCON

  (GMT+08:00) 2019-11-13 08:12:23

  Mshambiliaji wa Liverpool Mohamed Salah atakosa michuano ya kufuzu kombe la Mataifa ya Afrika AFCON huko Misri dhidi ya Kenya na Comoro kutokana na jeraha la kifundo cha mguu. Mo mwenye miaka 27 alibadilishwa dakika ya 87 kwenye mchezo wa ligi ya Premier walipovaana na Manchester City na kuondoka na zawadi ya magoli 3-1 siku ya Jumapili. Salah alikutana na kikosi cha Misri jana Jumanne kwaajili ya kujaribiwa jeraha lake na baadaye Misri kutoa taarifa kuwa jeraha lake litahitaji muda wa kutibiwa ili kupona. Salah alikosa mchezo wao waliotoka sare dhidi ya Manchester United mwezi Oktoba Oktoba baada ya mchezaji wa Leicester Hamza Choudhury kumjeruhi sehemu hiyohiyo ya mguu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako