• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kamisheni ya kujenga amani ya UM yapongeza mageuzi yanayoendelea Ethiopia

  (GMT+08:00) 2019-11-13 08:22:57

  Kamisheni ya kujenga amani ya Umoja wa Mataifa imesema mageuzi yanayoendelea nchini Ethiopia yameifanya nchi hiyo kuwa "mnara wa matumaini".

  Wajumbe wa kamisheni hiyo wamesema hayo walipokutana na rais Sahle-Work Zewde wa Ethiopia mjini Addis Ababa. Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Rais wa Ethiopia imesema kamisheni hiyo pia imesisitiza umuhimu wa kuyahusisha malengo ya kitaifa kwenye mchakato wa kujenga amani.

  Akizungumza kwenye mkutano huo, rais Zewde amesisitiza umuhimu wa kuzingatia hali halisi na uzoefu wa wenyeji wakati wa kuweka mipango ya kujenga amani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako