• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wanawake wa Namibia kunufaika na miradi iliyofadhiliwa na China

  (GMT+08:00) 2019-11-13 08:34:16

  Ofisa mwandamizi wa serikali ya Namibia ameishukuru serikali ya China kwa msaada wa dola za kimarekani elfu 40 kwa ajili ya wanawake walioko kwenye mazingira magumu kuweza kununua vyerehani.

  Waziri wa usawa wa kijinsia na maendeleo ya watoto Bibi Doreen Sioka amesema wanawake waliopokea vyerehani vilivyonunuliwa kwa fedha hizo maisha yao sasa yanabadilika.

  Amesema wanawake hao sasa wanaweza kujitegemea baada ya kupata msaada huo uliowawezesha kuendeleza biashara zao kwenye ushonaji na utengenezaji wa nguo. Bibi Sioka amesema wote waliopokea msaada huo wanatoka kwenye mazingira magumu lakini sasa maisha yao yameboreka, na kwamba Namibia itaendelea kuwawezesha wanawake.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako