• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa maadhimisho ya miaka 25 ya kufanyika kwa mkutano wa kimataifa wa idadi ya watu na maendeleo wafunguliwa Nairobi

  (GMT+08:00) 2019-11-13 08:43:23

  Mkutano wa kilele wa maadhimisho ya miaka 25 ya kufanyika kwa mkutano wa kimataifa wa idadi ya watu na maendeleo ulifunguliwa jana huko Nairobi, ambapo washiriki wanajadili masuala mbalimbali ikiwemo kinga na matibabu ya ugonjwa wa Ukimwi, ulinzi wa watoto wa kike, afya ya uzazi, na kuzeeka kwa watu.

  Mkutano huo wa siku tatu unaendeshwa na serikali za Kenya na Denmark, pamoja na Shirika la idadi ya watu la Umoja wa Mataifa. Wajumbe zaidi ya 7,000 kutoka nchi mbalimbali duniani wamehudhuria mkutano huo.

  Rais Kenyatta Uhuru wa Kenya kwenye ufunguzi wa mkutano huo amezitaka nchi mbalimbali ziongeze uwekezaji kwenye huduma za afya ya uzazi kwa wanawake, na kupata mafanikio zaidi kupitia utafiti, teknolojia na uvumbuzi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako