• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika Kusini yaahidi kuimarisha uhusiano kati ya nchi za BRICS

    (GMT+08:00) 2019-11-13 08:50:24

    Afrika Kusini imeahidi kuimarisha ushirikiano kati ya nchi za BRICS, hasa katika biashara na uwekezaji. Ikulu ya Afrika Kusini imesema uanachama wa Afrika Kusini katika kundi la nchi za BRICS unaiwezesha kutumia zana zenye nguvu katika changamoto tatu za ukosefu wa ajira, umaskini na kutokuwa na usawa kwa kupitia biashara, uwekezaji, utalii, ujenzi wa uwezo, ustadi na uhamishaji wa teknolojia.

    Taarifa hiyo imetolewa kabla ya rais Cyril Ramaphosa kwenda Brasilia, Brazil kuhudhuria mkutano wa kilele wa 11 wa BRICS unaofanyika leo na kesho.

    Kwenye taarifa hiyo, msemaji wa rais wa Afrika Kusini Bw. Khusela Diko amesema, ushiriki wa rais Ramaphosa kwenye mkutano una lengo la kuchangia mwelekeo wa kundi la BRICS, kuimarisha uhusiano kati ya nchi za BRICS na ushirikiano wa kunufaishana kupitia ushirikiano wa nguzo nne, hasa wa biashara na uwekezaji ndani ya BRICS, pamoja na kuhakikisha utekelezaji wa matokeo yaliyofikiwa kwenye mkutano wa kilele wa 10 wa BRICS uliofanyika mwaka jana nchini Afrika Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako