• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakimbizi wa DRC wakumbwa na ukiukwaji wa haki za binadamu

    (GMT+08:00) 2019-11-13 08:57:36

    Msemaji wa Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR Bw. Babar Baloch, amesema mamia ya maelfu ya wakimbizi walioko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC wanakabiliwa na vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu bila ulinzi.

    Amesema wakimbizi takriban laki 3 wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto wamekimbia makazi yao kutokana na kushambuliwa na makundi mbalimabli yenye silaha katika mikoa ya Ituri na Kivu Kaskazini mwezi Juni mwaka huu. Kwa sasa kuna wakimbizi milioni 4 nchini humo, idadi ambayo inachukua asilimia 10 ya wakimbizi kote duniani.

    Takwimu kutoka UNHCR zinaonyesha kuwa matukio yasiyopungua elfu moja ya ukiukwaji wa haki za binadamu yameshuhudiwa mwezi uliopita katika mikoa hiyo miwili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako