• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki za Zimbabwe zaanza kutoa noti mpya

    (GMT+08:00) 2019-11-13 09:12:15

    Benki za Zimbabwe zimeanza kutoa noti na sarafu mpya zilizotolewa na benki kuu ya nchi hiyo RBZ ili kupunguza ukosefu wa sasa wa pesa taslim.

    Watu walitarajia kuanza kupata pesa hizo kuanzia jumatatu kutokana na tangazo la awali la benki kuu, lakini noti hizo hazikupatikana kutokana na benki kutumia siku hiyo nzima kukusanya pesa hizo kutoka benki kuu.

    Hata hivyo baadhi ya wateja wamelalamika kuwa kiwango cha chini cha kuchukua pesa katika benki yake ni dola 50 kwa wiki, ingawa kiwango cha juu zaidi cha kuchukua pesa ni dola 300. Mhudumu mmoja wa benki ya biashara amesema, wanatarajia kuongeza kiwango cha kuchukua pesa, kama wakiendelea kupata pesa za kutosha kutoka benki kuu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako