• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • IOM yatoa mpango wa kijamii kwa watu waliopotea makazi nchini Ethiopia

  (GMT+08:00) 2019-11-13 09:12:31

  Shirika la kimataifa la uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM limetoa mpango mpya wa kijamii kwa watu wanaopotea makazi katika jimbo la Somali lililoko kusini mashariki mwa Ethiopia.

  Shirika hilo limetoa taarifa ikisema, wenzi wa kibinadamu ikiwemo IOM sasa wanaongeza matumizi ya mpango wenye msingi wa jamii kuunga mkono mpango wa kurejesha wakimbizi wa serikali ya Ethiopia, kuimarisha urejeaji endelevu, uponyaji na uunganisho la jamii.

  Hatua hiyo imechukuliwa baada ya nchi hiyo kurekodi watu wapatao milioni 3.40 waliopoteza makazi nchini humo hadi mwezi wa Machi mwaka huu kutokana na mapigano ya kikabila na mabadiliko ya kimazingira katika mwaka uliopita.

  Tangu mwezi wa Aprili mwaka 2019, serikali ya Ethiopia imeshiriki katika mpango ambao unataka kurejesha, kuhamisha na kujumuisha waliopotea makazi kwenye jamii, ili kuwarejesha maelfu ya wakimbizi wa ndani kurudi makwao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako