• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watoto 7,640 wa Sudan Kusini wafariki kutokana na nimonia mwaka 2018

    (GMT+08:00) 2019-11-13 09:21:48

    Ripoti iliyotolewa na Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF na mashirika ya hisani kwa watoto imesema ugonjwa wa nimonia unasababisha kifo cha mtoto mmoja kwa saa nchini Sudan Kusini, na mwaka jana watoto 7,640 chini ya umri wa miaka mitano walifariki.

    Shirika hilo limesema mwaka 2018 nimonia ni ugonjwa ulioongoza kusababisha vifo vya watoto nchini Sudan Kusini, na kusababisha asilimia 20 ya vifo vya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano kutokana na ukosefu wa usawa, umaskini na ukosefu wa upatikanaji wa huduma za afya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako