• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makampuni ya nchi za BRICS yatumai ukuaji wa mfululizo wa ushirikiano wa uchumi na biashara

    (GMT+08:00) 2019-11-13 16:58:58

    Mkutano wa 11 wa viongozi wa nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini zinazounda kundi la BRICS utafanyika kwa siku mbili kuanzia leo nchini Brazil, ukiwa na kauli mbiu ya "Ukuaji wa uchumi: Kuanzisha mustakabali wenye uvumbuzi". Wakuu wa makampuni ya nchi za kundi hilo walioshiriki kwenye Maonesho ya pili ya Kimataifa ya Uingizaji wa Bidhaa za nje ya China wanatumai kuwa, ushirikiano wa uchumi na biashara kati ya nchi hizo utaimarika siku hadi siku.

    Brazil ni nchi ya kwanza ya Latin-Amerika iliyoanzisha uhusiano wa wenzi wa kimkakati kwa pande zote na China, na China imekuwa mwenzi mkubwa zaidi wa kibiashara wa Brazil, pia ni nchi inayonunua bidhaa zake kwa wingi zaidi duniani kwa miaka 10 mfululizo. Takwimu zinaonesha kuwa, mwaka jana thamani ya biashara kati ya China na Brazil ilizidi dola za kimarekani bilioni 100. Mkurugenzi wa idara ya mambo ya kimataifa ya Shirikisho la Viwanda la jimbo la Sao Paulo nchini Brazil Bw. Thomas Sanoto amesema, Brazil inatumai kukuza ushirikiano wa uchumi na biashara na China. Anasema,

    "Maonesho ya Kimataifa ya Uingizaji wa Bidhaa za Nje ya China yanaiambia dunia kuwa, China si kama tu inauza bidhaa zake kwa nchi nyingine duniani, bali pia inapenda kununua bidhaa kutoka nchi nyingine. Kwa nchi yetu Brazil, hata wafanyabiashara wetu wa asali na karanga wameingia katika soko la China."

    Vyakula maalumu na anuwai ya usanii vya India vinajulikana nchini China. Mkuu wa kampuni moja ya vyakula ya India Bw. Hemant Motwani anasema,

    "Tumekuja kutafuta fursa ya ushirikiano katika soko la China. Tunajua maonesho hayo ni jukwaa kubwa, haswa kwa uingizaji wa bidhaa za nje nchini China. Tunatumai kutafuta fursa ya kibiashara pamoja na wenzi wa China."

    Wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Uingizaji wa Bidhaa za Nje ya China yaliyofanyika mjini Shanghai, vyakula vya Russia viliwavutia wachina wengi. Wafanyakazi wa Kampuni ya Vyakula ya Laycy Queen ya Russia waliwaambia wanahabari kuwa kampuni hiyo inapenda sana soko la China, na itaanzisha maduka mengi nchini China.

    Ikiwa nchi ya pili kwa ukubwa wa uchumi barani Afrika, Afrika Kusini imekuwa mwenzi wa kwanza wa kibiashara wa China barani Afrika kwa miaka 9 mfululizo. Mtendaji mkuu wa Shirikisho la Aluminum la Afrika Kusini Bw. Muzi Manzi anasema,

    "China ina soko kubwa na fursa nyingi za kibiashara. Natumai kupata wenzi hapa katika shughuli za Aluminum, na kuwauzia bidhaa zetu bora."

    Katika miaka kadhaa iliyopita, ushirikiano kati ya nchi za BRICS umeendelea kwa mfululizo. Takwimu zinaonesha kuwa, uchumi wa jumla wa nchi hizo unachukua asilimia 23.52 ya uchumi wa dunia, na nchi hizo zimekuwa nguvu ya kiujenzi ya kuhimiza ukuaji wa uchumi wa dunia, kukamilisha usimamizi wa mambo ya kimataifa, na kuhimiza uhusiano wa kidemokarasia duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako