• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Samatta aionya Stars

  (GMT+08:00) 2019-11-13 18:18:19
  Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Samatta amewaonya wachezaji wenzake wa timu hiyo kutowadharau Equatorial Guinea ambao watachuana nao ijumaa wiki hii katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwenye mechi ya kwanza ya kuwania kufuzu fainali za AFCON 2021. Samatta ametoa onyo hilo ili kuepuka yaliyotokea mwaka jana katika mechi kati ya timu hiyo na Lesotho. Wakati huohuo, Kocha wa Taifa Stars Etiene Ndayiragije, amemruhusu kiungo wa klabu ya Simba Jonas Mkude kuondoka kwenye kikosi hicho kwenda kushughulikia masuala yake ya kifamilia. Mkude aliomba ruhusa kwa kocha huyo kutojiunga na wenzake ili kushughulikia masuala ya kifamilia, ruhusa ambayo alipewa kabla ya kuanza kwa kambi.
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako