• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ubaguzi na mantiki yenye makosa haziwezi kubadilisha hali halisi ya kuwepo kwa China moja

  (GMT+08:00) 2019-11-13 19:36:10

  Msemaji wa ofisi ya mambo ya mkoa wa Taiwan ya Baraza la Serikali la China Bw. Ma Xiaoguang leo amesema kuwa, kuna China moja tu duniani, na mkoa wa Taiwan ni sehemu moja ya China, hali halisi hii inayokubaliwa na jumuiya ya kimataifa haibadiliki na baadhi ya wanasiasa wa Marekani kutokana na ubaguzi na mantiki yenye makosa.

  Bw. Ma amesema hayo kufuatia habari kuwa, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo hivi karibuni alisema, Marekani ilipunguza kiwango cha uhusiano wake na Taiwan kwa muda mrefu kwa ajili ya kurekebisha uhusiano kati yake na China bara, na kutatua suala la Taiwan kwa njia ya amani, kitendo ambacho ni kinyume na maadili ya Marekani na demokrasia ya nchi za magharibi.

  Bw. Ma ameitaka Marekani itekeleze kanuni ya kuwepo kwa China moja na taarifa tatu za pamoja zilizotolewa na China na Marekani, na kujitahidi kutatua masuala yanayohusisha Taiwan kwa mwafaka ili kuepuka kuharibu uhusiano kati ya China na Marekani, na amani na utulivu ya sehemu ya mlango bahari wa Taiwan.

  Pia Bw. Ma amesema, hatua 26 zilizotolewa na China bara kwa kuhimiza ushirikiano na mawasiliano ya uchumi na utamaduni kati ya pande hizo mbili zitaleta fursa na manufaa zaidi ya maendeleo kwa watu wa mkoa wa Taiwan.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako