• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Xi Jinping wa China afanya mazungumzo na mwenzake wa Brazil Jair Bolsonaro

  (GMT+08:00) 2019-11-14 08:09:54

  Rais Xi Jinping wa China amefanya mazungumzo na mwenzake wa Brazil Jair Bolsonaro jana Jumatano mjini Brasilia.

  Kwenye mazungumzo yao rais Xi amesisitiza kuwa China na Brazil ambazo zote ni nchi kubwa, zinapaswa kudumisha dhamira ya kimkakati, kushikilia kuheshimiana, kutendeana kwa usawa, kuimarisha mawasiliano na kuinua kiwango cha kuaminiana. Amesema nchi hizo pia zinapaswa kufunguliana soko, na kutafuta kujenga njia za uhakika na za moja kwa moja za ugavi wa bidhaa za kimsingi zikiwemo mazao ya kilimo, madini ya chuma na mafuta ghafi. Rais Xi ameitaka Brazil ishirikiane na China katika kuhimiza mawasiliano na ushirikiano wa pande zote kati ya China na nchi za Latin Amerika, kushikilia utaratibu wa pande nyingi, kujenga uchumi wa dunia ulio wazi na kulinda kwa pamoja haki halali ya nchi zinazoendelea za kujiendeleza. Pia ameongeza kuwa China inaunga mkono Brazil kuandaa Mkutano wa Kilele wa BRICS, na inapenda kushirikiana na pande mbalimbali kufanikisha mkutano huo.

  Rais Jair Bolsonaro amesema, China ikiwa ni mwenzi mkubwa wa kwanza wa kibiashara kwa Brazil, ushirikiano kati yake na Brazil una umuhimu mkubwa kwa maendeleo ya Brazil katika siku zijazo. Amesema Brazil inakaribisha kampuni za China kuwekeza nchini humo, na kuimarisha ushirikiano katika sekta za miundombinu, madini ya chuma, na mafuta na gesi asilia. Rais Bolsonaro pia ameishukuru China kwa uaminifu na urafiki wake, na Brazil inatilia maanani kupanua ushirikiano na China katika nyanja mbalimbali, na kuimarisha urafiki kati yao, ili kunufaisha zaidi watu wa nchi hizo mbili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako