• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ofisa wa Umoja wa Afrika asema fedha za ndani ni muhimu katika kuhimiza uzazi wa mpango

  (GMT+08:00) 2019-11-14 08:26:23

  Kamishna wa mambo ya kijamii wa Umoja wa Afrika anayeshughulikia mambo ya kijamii Bibi Amira El Fadil, amesema uhamasishaji mkubwa wa fedha za ndani tofauti na hali ya sasa ya kutegemea fedha kutoka kwa wahisani, linaweza kuwa suluhisho la muda mrefu la ukosefu wa njia za kuzuia uzazi kwa nchi za Afrika.

  Akiongea kwenye mkutano wa kimataifa wa idadi ya watu na maendeleo (ICDP 25) unaoendelea mjini Nairobi, Bibi Amira amesema bara la Afrika linatakiwa kuachana na utegemezi wa wahisani wa nje kwenye kutoa huduma za uzazi wa mpango, kwa kuhimiza makampuni ya kienyeji kuwekeza kwenye utafiti, uzalishaji na usambazaji wa bidhaa za uzazi wa mpango.

  Amesema kuwekwa kwa msimamo wa pamoja wa Idadi ya watu na maendeleo wa nchi za Afrika kumepitishwa na Umoja wa Afrika, kutahimiza matumizi ya fedha za ndani kwenye huduma za uzazi wa mpango.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako