• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kampeni ya dunia yahimiza hatua kuchukuliwa kupambana na ukatili wa kijinsia

  (GMT+08:00) 2019-11-14 08:26:55

  Waziri wa jinsia na vijana wa Kenya Bibi Margaret Kobia amesema kuna haja ya serikali za nchi mbalimbali duniani kupitisha sheria za kutoa adhabu na kuwekeza kwenye uhamasishaji mashinani ili kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na wasichana vinavyozidi kuongezeka.

  Bibi Kobia amesema uharaka wa kukomesha vitendo vyote vya ukatili dhidi ya wanawake na wasichana ni muhimu, katika wakati huu ambapo vitendo hivyo vinaongezeka na kutishia kuondoa mafanikio yaliyopatikana kwenye kuleta usawa wa kijinsia.

  Kamishna wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Haki za binadamu Bibi Michelle Bachelet, amesema kuwawezesha wanawake kupitia elimu, ujuzi, ajira na huduma za afya ya uzazi kutasaidia kuleta msukumo kukomesha mabavu ya kijinsia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako