• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Tanzania yasema watumiaji wa simu zisizosajiliwa hawatazuiwa baada ya kikomo cha Desemba

    (GMT+08:00) 2019-11-14 08:51:09

    Waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania Bw. Kangi Lugola ameliambia bunge la nchi hiyo kuwa watumiaji wa simu zisizosajiliwa ambao walishindwa kusajili kadi zao za SIM kwa njia ya kibiometrika hadi kikomo cha Desemba 31, hawatazuiwa.

    Bw. Lugola amesema watumiaji wa simu wataendelea kufurahia huduma za mawasiliano hata baada ya kikomo, huku akiongeza kuwa hakuna kadi yoyote ya SIM ambayo itazimwa na pia hakuna yeyote atakayezuiwa huduma za simu kutokana na kutosajili.

    Bw. Lugola ametoa taarifa hiyo siku mbili baada ya mamlaka ya mawasiliano ya nchi hiyo kutangaza kuwa watumiaji wa simu wapatao milioni 31 ambao hawajasajili kwa njia ya kibiometrika wako hatarini kuzuiwa baada ya ya Desemba 31.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako