• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Arsene Wenger aramba dili nono FIFA

  (GMT+08:00) 2019-11-14 09:31:06

  Kocha wa zamani wa Arsenal, Mfaransa Arsene Wenger, ameramba dili nono kwa kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa maendeleo ya Soka Duniani. (FIFA's chief of global football development). Rais wa FIFA Gian Infantino amesema anaamini uzoefu na weledi wa Wenger utasaidia katika eneo la Ufundi na Utunzi wa sheria. Hatua hiyo inamaliza uvumi wa kumuunganisha Mfaransa huyo, mwenye miaka 70, na kurudi kama bosi wa Bayern Munich. Wenger aliondoka Gunners mnamo Mei 2018, baada ya kutumikia kwa miaka 22, akishinda mataji matatu ya Ligi Kuu Uingereza na makombe saba ya FA. Sasa atakuwa mwanachama wa jopo la kiufundi la Bodi ya Chama cha Soka la Kimataifa, na mwenyekiti wa bodi ya masomo ya kiufundi zaidi Fifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako