• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkuu wa Shirika Kuu la Utangazaji la China ahojiwa na mwanahabari wa Brazil

  (GMT+08:00) 2019-11-14 17:13:19

  Gazeti kubwa nchini Brazil Folha de Sao Paulo limetoa makala ya mahojiano iliyofanya na mkuu wa Shirika Kuu la Utangazaji la China Bw. Shen Haixiong ambayo kichwa chake ni "Hongkong kwenye vyombo vya habari iko mbali sana na ukweli".

  Makala hiyo inasema Shirika Kuu la Utangazaji la China ni chombo kikubwa zaidi cha habari duniani, na mkuu wake Bw. Shen Haixiong anaona kuwa, vurugu za Hongkong si maandamano ya kawaida, bali ni kitendo cha kigaidi. Bw. Shen amekosoa vyombo vya habari vya nchi za magharibi kwa kutoripoti hali halisi ya China na kusema, kwenye ripoti zao, vyombo hivyo haswa vya Marekani vinachagua baadhi ya mambo ambayo hayaoneshi hali halisi. Ameongeza kuwa mwishoni mwa wiki iliyopita, waandamanji walimchoma moto mzee mmoja aliyekabiliana nao, hivyo anaona kuwa vitendo vya kimabavu vya baadhi ya waandamanaji ni vya kigaidi.

  Bw. Shen ambaye yupo ziarani Brazil akifuata rais Xi Jinping wa China alisaini makubaliano ya ushirikiano na Chombo cha Habari cha Bandeirantes de Comunicacao cha Brazil, akisema huo ni mwanzo wa ushirikiano, na pande hizo mbili zitasukuma mbele ushirikiano katika sekta mbalimbali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako