• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • NDONDI: Mwakinyo, Mfilipino waanza tambo

  (GMT+08:00) 2019-11-14 18:28:11

  Bondia Arnel Tinampay wa Philippines amemtaka Hassan Mwakinyo, bondia wa Tanzania, kujiandaa kwa kipigo kwa kuwa anafahamu ubora na udhaifu wake. Vyombo vya habari vya Philippines vimemnukuu bondia huyo akitamba kuwa atashinda pambano hilo litakalofanyika Novemba 29 jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tinampay, bondia namba moja nchini humo kwenye uzani wa super welter amesema anakwenda Tanzania kuendeleza wimbi la ushindi. Wakati bondia huyo akijitapa, bondia Hassan Mwakinyo amewatoa hofu Watanzania kuhusu pambano hilo na kusema anafanya mazoezi mazuri ya kutosha kumpatia ushindi. Mwakinyo ambaye ameweka kambi yake mkoani Tanga, alisema maandalizi yake yanaendelea vizuri hivi sasa kwani anazingatia ushauri aliopewa na mwalimu wake ambapo amemtaka afanye mazoezi pamoja na kuchukua mapumziko.
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako