• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China atarajia sekta za viwanda na biashara kuchukua fursa kusaidia maendeleo yenye ubora wa juu ya nchi za BRICS

  (GMT+08:00) 2019-11-14 18:37:28

  Rais Xi Jinping wa China amehutubia hafla ya kufungwa kwa kongamano la viwanda na biashara la nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini zinazounda kundi la BRICS lililofanyika katika mji mkuu wa Brazil, Brasilia

  Rais Xi amesema, anatarajia sekta za viwanda na biashara kuchukua fursa hiyo kukabiliana na changamoto, kutambua uhusiano wa wenzi wa mapinduzi mapya ya kiviwanda wa nchi za BRICS kama injini ya ushirikiano wa uchumi kati yao, ili kusaidia maendeleo yenye ubora wa juu ya uchumi wa nchi hizo tano.

  Kongamano hilo ni shughuli muhimu ya mkutano wa viongozi wa nchi za BRICS, pia ni jukwaa muhimu kwao kujadiliana na kushauriana kuhusu masuala wanayofuatilia zaidi. Sherehe hiyo ilifanyika katika kituo cha mikutano ya kimataifa cha Brazil, na kuwashirikisha marais Jair Bolsonaro wa Brazil, Vladmir Putin wa Russia, Xi Jinpingi wa China, Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, waziri mkuu wa India Narendra Modi na wajumbe wapatao 600 wa sekta za viwanda na biashara wa nchi za BRICS.

  Kwenye hotuba yake, rais Xi amesema, hali ya dunia hivi sasa imebadilika na kuwa na fursa na changamoto nyingi. Nguvu za duru mpya ya mageuzi ya teknolojia na viwanda imeanza kutia nguvu kwenye maendeleo ya uzalishaji, jamii na uchumi. Wakati huohuo, mfumo wa kujilinda kibiashara na vitendo vya upande mmoja unaendelea kujitokeza na kuharibu biashara ya kimatiafa na uwekezaji, na kuongeza shinikizo katika kushuka kwa uchumi wa dunia. Rais Xi amesema, makampuni yakiwa na imani, soko litakuwa na nguvu, na kuhimiza sekta za viwanda na biashara kushiriki na kusukuma mbele ushirikiano wa uchumi kati ya nchi za BRICS.

  "Natarajia marafiki wa sekta za viwanda na biashara kuchukua fursa hiyo kukabiliana na changamoto, kuendelea kutumia manufaa yenyewe, kushiriki na kusukuma mbele ushirikiano wa uchumi kati ya nchi za BRICS, na kujitahidi kuwekeza katika nchi za BRICS ili kutoa mchango halisi katika kuhimiza maendeleo na ajira."

  Rais Xi pia amesema, uhusiano wa wenzi wa magezui mapya ya kiviwanda wa nchi za BRICS ni muhimu katika ushirikiano wa uchumi wa nchi hizo katika kipindi kijacho.

  "Makampuni yanapaswa kuthubutu kufanya majaribio, kuunganisha ushirikiano wa makampuni pamoja na uhusiano wa wenzi wa mapinduzi mapya ya kiviwanda ili kujitahidi kupata mafanikio katika uvumbuzi, uchumi wa kidijitali, uchumi wa mazingira safi na kusaidia kwenye maendeleo yenye ubora wa juu ya uchumi wa nchi hizo tano."

  Rais Xi amesema, hivi sasa, utandawazi wa uchumi unakabiliwa na matatizo. Pande mbalimbali zinapaswa kugundua mambo yanayozuia mawasiliano ya uwekezaji wa kibiashra na kutoa utatuzi unaofaa ili kuzisaidia serikali kuelewa zaidi matakwa ya soko na kuongeza ufanisi wa sera. Rais Xi amesisitiza kuwa, maendeleo ya China ni fursa kwa dunia.

  "Katika siku za baadaye, nia ya China ya kufungua mlango na mwelekeo mzuri wa uchumi wa China hautabadilisha.\ Tutaendelea kufungua soko, kuongeza uingizaji bidhaa za nje, kuendelea kuboresha mazingira ya biashara ili kutoa fursa nzuri kwa maendeleo ya makampuni. Ujenzi wa 'Ukanda Mmoja na Njia Moja' umeingia kwenye kipindi cha maendeleo yenye ubora wa juu. Natarajia wamiliki wa makampuni watachukua fursa hiyo kushiriki kwa hamasa ili kupata mafanikio zaidi ya ushirikiano"

  Rais Xi na mke wake Bibi Peng Liyuan, pia walihudhuria dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na rais wa Brazil kukaribisha viongozi wa nchi za BRICS.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako