• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping asema jukumu la dharura kwa Hongkong ni kuondoa ghasia na kurejesha utaratibu

    (GMT+08:00) 2019-11-15 08:42:51

    Rais Xi Jinping wa China ameeleza msimamo thabiti wa serikali ya China kuhusu hali ya sasa ya Hongkong, alipohudhuria mkutano wa 11 wa viongozi wa nchi za BRCIS unaofanyika nchini Brazil.

    Rais Xi amesema, vitendo vya uhalifu wa kimabavu vinavyoendelea kutokea mkoani Hongkong, vimehujumu vibaya utawala wa kisheria na utaratibu wa kijamii, vimeharibu vibaya ustawi na utulivu wa Hongkong, na vimekiuka vibaya mstari mwekundu wa sera ya "Nchi Moja, Mifumo Miwili". Hivi sasa Jukumu la dharura kwa Hongkong ni kuondoa ghasia na vurugu na kurejesha utaratibu. Amesema serikali kuu ya China itaendelea kumwunga mkono kithabiti ofisa mkuu kuongoza serikali ya Hongkong kutekeleza utawala wa kisheria, kuunga mkono kithabiti polisi ya Hongkong kutekeleza sheria kwa hatua madhubuti, na kuunga mkono taasisi za kisheria za Hongkong kuwaadhibu wahalifu kwa mujibu wa sheria. Amesisitiza kuwa serikali kuu ya China ina dhamira thabiti ya kulinda mamlaka ya nchi, usalama na maslahi ya maendeleo, kutekeleza mkakati wa "Nchi moja Mifumo miwili", na kupinga kithabiti uingiliaji wa nje kwenye mambo ya Hongkong.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako