• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Teruyo Tanaka ashinda medali ya fedha akiwa na umri wa miaka 60

    (GMT+08:00) 2019-11-15 09:10:53

    Mjapani Teruyo Tanaka ameshinda mbio za kitengo cha T52 m100 na kujizolea medali ya fedha kwenye mashindano ya Mabingwa wa Riadha ya Walemavu Duniani akiwa na umri wa miaka 60. Tanaka, aliyeanza kushiriki michezo mwaka 1988, ameandikisha muda bora katika msimu kwa kutumia sekunde 22.85 na kumaliza wa pili nyuma ya Mmarekani Kerry Morgan, mwenye miaka 45, huko Dubai. Alishinda dhahabu mita 800 katika michezo ya walemavu ya Atlanta 1996 na kujizolea medali nyingi zaidi katika michezo ya Sydney 2000 na Beijing 2008. Bi Tanaka amesema hakutaka kushindwa na wanariadha wenye umri mdogo. Michuano ya wanawake ya T52 m100 bado haijathibitishwa kwenye mbio za walemavu za Tokyo 2020, lakini Bi Tanaka amesema itakuwa heshima kushindana katika ardhi ya nyumbani. Tanaka sio mwanariadha mzee zaidi kwenye michuano ya Dubai. Bali heshima hiyo inakwenda kwa Mjapani mwenziwe Toshie Oi, aliyemaliza watano katika kitengo cha T53 akiwa na umri wa miaka 71. Na mdogo kabisa ni Mmarekani mwenye miaka 14 ambaye alimaliza wa saba katika kitengo cha T63 kuruka juu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako