• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China akutana na mwenzake wa Afrika Kusini

  (GMT+08:00) 2019-11-15 09:20:54

  Rais Xi Jinping wa China huko Brasilia amekutana na mwenzake wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, na kumwambia kuwa China na Afrika Kusini zikiwa nchi muhimu zinazoendelea na soko jipya linalojitokeza, zinabeba majukumu ya ndani ya kuendeleza uchumi na kuboresha maisha ya watu, na majukumu ya nje ya kulinda kithabiti mfumo wa pande nyingi na kupinga hatua za upande mmoja na vitendo vya umwamba.

  Amesema China inapenda kushirikiana na Afrika Kusini kulinda na kuendeleza kithabiti uhusiano wa kimkakati na kiwenzi wa pande zote kati ya nchi hizo mbili.

  Rais Ramaphosa amepongeza maadhimisho ya miaka 70 tangu Jamhuri ya Watu wa China ilipoanzishwa,,pamoja na mafanikio waliyopata watu wa China chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China, na kusema kuwa Afrika Kusini inaunga mkono kithabiti maendeleo ya China.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako