• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China ahudhuria na kuhutubia mkutano wa 11 wa viongozi wa BRICS

    (GMT+08:00) 2019-11-15 09:25:00

    Mkutano wa 11 wa viongozi wa nchi za BRICS ulifanyika jana mjini Brasilia, Brazil, ukiendeshwa na rais Jair Bolsonaro wa Brazil na kuhudhuriwa na marais wa China, Russia, Afrika Kusini na waziri mkuu wa India. Viongozi wa nchi hizo tano wamebadilishana maoni kwa kina na kufikia makubaliano kuhusu ushirikiano kati ya nchi za BRICS na masuala makubwa ya kimataifa wanayofuatilia kwa pamoja.

    Akitoa hotuba kuhusu kufanya juhudi kwa pamoja kwa ajili ya kufungua ukurasa mpya wa ushirikiano, rais Xi Jinping wa China amesisitiza kuwa nchi za BRICS zinapaswa kubeba wajibu wao, kutetea na kutekeleza taratibu za pande nyingi, kujenga mazingira ya kiusalama yenye amani na utulivu, zinapaswa kutumia vizuri fursa za kizama za kufanya mageuzi na uvumbuzi, na kusukuma mbele ushirikiano kati ya nchi za BRICS kwenye mapinduzi mapya ya kiviwanda. Amesema nchi za BRICS pia zinapaswa kufundishana na kuendelea kupanua mawasiliano ya kiutamaduni kati yao. Rais Xi amesisitiza kuwa China itafungua mlango zaidi, kusukuma mbele ujenzi wenye ubora wa "Ukanda mmoja, Njia moja", na kujitahidi kuhimiza ujenzi wa Jumuiya ya nchi za Asia na Pasifiki yenye hatma ya pamoja na jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako