• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China atetea utaratibu wa pande nyingi kwenye mkutano wa BRICS

    (GMT+08:00) 2019-11-15 18:09:52

    Mkutano wa 11 wa viongozi wa nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini zinazounda kundi la BRICS umefanyika mjini Brasilia, Brazil, na kuhudhuriwa na marais Jair Bolsonaro wa Brazil, Xi Jinping wa China, Vladmir Putin wa Russia, Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini na waziri mkuu wa India Narendra Modi. Rais Xi amehutubia ufunguzi wa mkutano huo akizihimiza nchi hizo kubeba majukumu ya kutetea na kutekeleza utaratibu wa pande nyingi.

    Kwenye hotuba yake, rais Xi amesisitiza kuwa nchi za BRICS zinapaswa kutetea na kutekeleza kivitendo utaratibu wa pande nyingi, kuanzisha mazingira ya usalama yenye amani na utulivu, na kutumia vizuri fursa za zama za sasa kufanya mageuzi na uvumbuzi. Pia kusukuma mbele kwa kina uhusiano wa wenzi wa mapinduzi mapya ya kiviwanda kati yao, kuhimiza kuigana na kufunzana, na kuongeza kina na upana wa mawasiliano ya watu na ustaarabu. Amesema China itashikilia kufungua mlango zaidi, kusukuma mbele ujenzi wa pamoja wenye sifa ya juu wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na kuhimiza kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ya sehemu ya Asia na Pasifiki na ya binadamu kwa ujumla.

    Rais Xi amesema mkutano huo umefanyika wakati uchumi wa dunia na hali ya kimataifa vinakabiliwa na mabadiliko muhimu, na kuhimiza nchi za BRICS zifuate mkondo wa kisasa, kusikiliza matakwa ya watu, kushikilia kujiendeleza, na kushirikiana bega kwa bega, ili kuwanufaisha wananchi wao, na kutafuta maendeleo kwa dunia nzima. Ametoa mapendekezo matatu: kukuanzisha mazingira ya usalama yenye amani na utulivu, kujitahidi kupata maendeleo ya kufungua mlango na yenye uvumbuzi katika siku za baadaye, na kuhimiza mawasiliano ya kuigana na kufunzana ya watu na ustaarabu.

    Aidha, rais Xi amesisitiza kuwa, China itaendelea kufungua mlango zaidi, kuongeza uingizaji bidhaa na huduma kutoka nchi za nje, kupunguza vizuizi vya soko dhidi ya uwekezaji wa nje, na kuimarisha ulinzi wa hakimiliki za kiubunifu.

    Nao viongozi wengine wamesema hivi sasa ongezeko la vitendo vya upande mmoja, na kujilinda kibiashara linatishia mamlaka na usalama wa nchi nyingi, hivyo nchi za BRICS zinapaswa kufuata moyo wa wenzi wa kimkakati kuongeza mawasiliano na ushirikiano, kulinda kanuni ya Umoja wa Mataifa na utaratibu wa kimataifa, na mfumo wa kibiashara wa pande nyingi ulio wazi na dhahiri na wenye haki, ili kulinda maslahi ya pamoja ya nchi zinazoendelea na nchi zilizoibuka kiuchumi.

    Rais Xi pia amehudhuria mazungumzo kati ya viongozi na wajumbe wa Kamati ya Viwanda na Biashara na Benki ya Maendeleo ya BRICS, akipongeza kazi za mashirika hayo mawili, na kuyahimiza kutoa mchango zaidi kwa ajili ya maendeleo ya uchumi na jamii ya nchi zinazoendelea na nchi zilizoibuka kiuchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako