• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • KUOGELEA: Sun Yang asema tabia ya DCA ilimfanya awe na wasiwasi

  (GMT+08:00) 2019-11-15 18:33:06

  Championi mara tatu wa kuogelea nchini China Sun Yang amesema, tabia ya Msaidizi wa Udhibiti wa Matumizi ya Dawa za Kuongeza Nguvu (DCA) ilimtia wasiwasi ambao ulimfanya akatae kuendelea na vipimo vya kuangalia kama anatumia dawa hizo. Sun amefikishwa mbele ya CAS leo wakati Mamlaka ya Kimataifa ya Kupambana na Matumizi ya Dawa za Kuongeza Nguvu (WADA) ikikata rufaa dhidi ya mwogeleaji huyo na FINA kutokana na uamuzi wa awali wa FINA unaompendelea Sun kuhusu tuhuma za kukiuka kanuni za kutumia dawa za kuongeza nguvu. Sun ameeleza sababu zake za kutotoa ushirikiano wakati wa vipimo vilivyofanywa na IDTM usiku wa Septemba 4, kwa kuwa alichukulia tabia ya Msaidizi wa Udhibiti wa Kutumia Dawa hizo kuwa haikuwa ya kitaaluma.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako