• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Misri kuwa mwenyeji wa duru mpya ya mazunguzo kuhusu suala la bwawa la Nile

  (GMT+08:00) 2019-11-17 17:13:24

  Wizara ya rasilimali maji ya Misri jana ilisema, Misri itakuwa mwenyeji wa duru mpya ya mazungumzo yanayoanza tarehe 2 na kumalizika tarehe 3 Disemba, na kurejesha tena majadiliano kuhusu mgogoro wa bwawa la GERD.

  Katika mkutano uliofanyika tarehe 6 Novemba, mawaziri wa mambo ya nje wa Misri, Ethiopia na Sudan wamekubaliana kufanya mikutano minne ya kiserikali ya mawaziri wa mambo ya maji, na benki ya Dunia na Marekani zitaziunga mkono na kuhudhuria mikutano zikiwa kama wakaguzi.

  Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo inasema, katika mkutano wa kwanza uliyofanyika Ijumaa na Jumamosi, mambo ya kiufundi kuhusu mchakato wa kujaza na kuendesha bwawa yamejadiliwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako