• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Msaada wa matibabu wa China kwa AU kuinua zaidi uwezo wake wa kukabiliana na mlipuko wa magonjwa

  (GMT+08:00) 2019-11-17 18:30:11

  Mkuu wa kamati ya Umoja wa Afrika anayeshughulikia mambo ya kijamii Bibi Amira Elfadil leo amesema, msaada wa matibabu wa China kwa Umoja wa Afrika utainua zaidi uwezo wa Umoja wa Afrika kukabiliana na mlipuko wa magonjwa.

  Bibi Amira amesema, msaada huo unahusu pande mbalimbali, na ulio muhimu zaidi ni wa kifedha na kiufundi ambao unainua ujenzi wa uwezo wa matibabu ya magonjwa ya maambukizi wa Umoja wa Afrika. Kutokana na msaada wa China, Umoja wa Afrika una mpango wa kujenga maabara kadhaa, ambazo zitakuwa sehemu ya makao makuu ya kituo cha udhibiti wa magonjwa cha Afrika kinachojengwa kwa msaada wa China.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako