• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • TENISI: Stefanos Tsitsipas amtoa kijasho chembamba Dominic Thiem na kuchukua taji la ATP Finals

  (GMT+08:00) 2019-11-18 08:29:27

  Mcheza tenisi kinda kutoka Ugiriki Stefanos Tsitsipas jana aliendeleza kichapo chake dhidi ya Dominic Thiem katika hatua ya fainali na kuvishwa taji la ATP Finals akiwa mchezaji mdogo kabisa katika miaka 18 iliyopita kwenye mtanange huo. Tsitsipas mwenye miaka, 21, alishinda 6-7 (6-8) 6-2 7-6 (7-4) na kunyanyua taji hilo kubwa katika kibarua chake. Thiem, mwenye miaka 26, ambaye katika seti ya kwanza alimdhibiti kisawasawa mpinzani wake, alianza kuporoka katika seti ya pili kabla ya kupambana tena katika seti ya tatu. Lakini Tsitsipas alilazimisha sare na hatimaye kushinda katika O2 Arena huko London. Tsitsipas ni mshindi mdogo kabisa wa mashindano hayo ya kumaliza msimu tangu Muaustralia Lleyton Hewitt mwaka 2001 na kuondoka na zawadi ya kitita cha pesa zaidi ya £2m.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako