• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sudan yafanya juhudi kuondokana na changamoto za kisiasa na kiuchumi

  (GMT+08:00) 2019-11-18 08:54:42

  Sudan inaendelea na juhudi za kukabiliana na changamoto za kisiasa na kiuchumi, siku 75 baada ya kuanzishwa kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa, huku wataalam wakiona kuwa mustakbali wa kisiasa wa nchi hiyo unategemea masuluhisho yenye ufanisi.

  Mwanauchumi wa Sudan Bw. Hamid Al-Amin amesema kwa sasa Sudan inasumbuliwa na kilichofanywa na utawala uliopita kwa muda wa miaka 30, na kufanya nchi isiwe na mtazamo usioeleweka kwenye mambo ya kiuchumi na kisiasa, huku ikiwa imetengwa.

  Amesema uchumi wa Sudan haiwezi kukua bila kutegemea nchi nyingine, na kuitaka serikali ifanye mabadiliko makubwa kiuchumi ili kuiweka Sudan kwenye njia sahihi ya maendeleo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako