• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Bw. Jack Ma ahimiza wajisiriamali vijana wa Afrika kwa tuzo ya pesa

  (GMT+08:00) 2019-11-18 08:55:23

  Mwanzilishi wa kampuni ya biashara ya mtandaoni ya China Alibaba, Bw. Jack Ma, amesema mfuko wake utaendelea kuwaunga mkono wajasiriamali vijana wa Afrika.

  Bw. Jack Ma amesema hayo baada ya kutoa tuzo zenye thamani ya dola milioni moja kwa wajasiriamali 10 vijana wa Afrika kwenye tuzo za kwanza za wajasiriamali kupitia mtandao wa internet, zilizotolewa jumamosi mjini Accra, Ghana.

  Akiongea kwenye hafla ya utoaji wa tuzo hizo, Bw. Jack Ma amesema kama Afrika ikitaka kuwa na ongezeko endelevu, jambo muhimu ni kwa wajasiriamali hao kuwa na njia za uvumbuzi.

  Rais Akufo-Addo wa Ghana amesema kwenye hafla hiyo kuwa ujasiriamali unatakiwa kuchukuliwa kwa umakini mkubwa ili kuhimiza utamaduni wa ujasiriliamali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako