• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Raia wajeruhiwa kwenye shambulizi la makombora dhidi ya Eneo la Kijani katikati mwa Baghdad

  (GMT+08:00) 2019-11-18 09:10:37

  Makombora mawili jana yalianguka katika Eneo la Kijani lenye ulinzi mkali katikati ya mji wa Baghdad, na raia mmoja amejeruhiwa kwenye shambulizi hilo.

  Shambulizi hilo lilitokea juzi jioni baada ya kombora moja kutua kwenye jengo la kampuni ya mawasiliano ya simu kwenye eneo la al-Karrada kando ya mashariki ya Mto Tigris, karibu na Eneo la Kijani ambako kuna nyumba za balozi na baadhi ya ofisi kuu za serikali ya Iraq.

  Mlipuko huo ulimjeruhi mhandisi aliyekuwa anafanya kazi katika kampuni hiyo na kusababisha uharibifu wa jengo hilo. Kombora lingine lilitua katika eneo hilo lakini halikuleta madhara.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako