• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Washiriki wa kimataifa wazipongeza Somalia na Kenya kusukuma mbele kurejesha uhusiano

    (GMT+08:00) 2019-11-18 09:20:28

    Washirika wa kimataifa wamekaribisha hatua zilizokubaliwa na viongozi wa Somalia na Kenya kurejesha uhusiano kati ya nchi hizo mbili, baada ya mgogoro wa kidiplomasia wa miezi kadhaa kuhusu haki ya mafuta.

    Washirika kutoka Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya, Umoja wa Mataifa, Marekani na jumuiya ya ushirikiano wa nchi za kiislam, wamesema hatua hizo zikiwemo kurejesha utoaji wa viza kwa wananchi wanapofika ni hatua muhimu ya kuimarisha uhusiano mzuri kati ya nchi hizo mbili.

    Habari zinasema rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na mwenzake wa Somalia Mohamed Farmajo walikutana na kufanya mazungumzo tarehe 14 Novemba pembezoni mwa mkutano wa kimataifa wa idadi ya watu na maendeleo mjini Nairobi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako