• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa nchi za Kiarabu AL wapongeza kurefushwa kwa muda wa UNRWA

  (GMT+08:00) 2019-11-18 09:56:51

  Umoja wa Nchi za Kiarabu AL umeupongeza Umoja wa Mataifa kwa kurefusha muda wa idhini ya Idara yake ya Misaada na Kazi kwa Wakimbizi wa Palestina katika sehemu ya Mashariki ya Karibu UNRWA kwa miaka mitatu. Msaidizi wa katibu mkuu wa Umoja wa nchi za Kiarabu Bw. Saeed Abu Ali amesema uamuzi huo wa Umoja wa Mataifa umeonesha nia na uungaji mkono wa jumuiya ya kimataifa kwa kazi muhimu za UNRWA. Uamuzi huo ulipitishwa Ijumaa iliyopita na Umoja wa Mataifa kwa kura za maoni, na kukubaliwa na nchi 170, huku ukipingwa na Marekani na Israel.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako