• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Polisi Ethiopia yawakamata Wabrazil watano kutokana na magendo ya dawa za kulevya

  (GMT+08:00) 2019-11-18 09:57:57

  Serikali ya Ethiopia imesema Wabrazil watano wamekamatwa kwa kutuhumiwa kujaribu kufanya magendo ya Cocaine kilo 47.4 kwa nchi kadhaa kupitia Ethiopia. Habari zilizotolewa na Shirika la Utangazaji la FANA zinasema, Cocaine hiyo ilikamatwa katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Bole mjini Addis Ababa, na kati ya watu waliokamatwa, wanne ni wanawake. Habari zinasema watuhumiwa watatu kutoka Brazil walikuwa wakielekea Kigali kupitia Addis Ababa, na wengine wakielekea Johannesburg, Afrika Kusini, na Bangkok, Thailand.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako