• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa na Sudan Kusini washirikiana kutoa chanjo ya kipindupindu kwa watu laki 1.44 nchini humo

    (GMT+08:00) 2019-11-18 10:13:44

    Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanashirikiana na wizara ya afya ya Sudan Kusini kuzindua mazoezi ya kutoa chanjo ya kipindupindu kwa watu laki 1.44 katika kaunti ya Renk.

    Shirika la Afya Duniani (WHO), Shirika la kuhudumia watoto UNICEF na shirika la MedAir yamesema raundi ya kwanza ya chanjo ya kipindupindu itaanza tarehe 18 hadi tarehe 23, mwezi huu. Raundi ya pili inapangwa kuanzisha tarehe 9, hadi tarehe 13, mwezi wa Desemba.

    Habari zinasema kaunti ya Renk ni moja ya kaunti zilizokumbwa na mlipuko wa kipindupindu kwa muda mrefu na kwa kiasi kubwa zaidi. WHO imesema hadi kufikia tarehe 12 Oktoba, watu 278 waliripotiwa kuambukizwa, wanane kati yao wamefariki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako