• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Misri yafanya sherehe ya kuadhimisha miaka 150 ya kufunguliwa kwa mfereji wa Suez

  (GMT+08:00) 2019-11-18 10:14:09

  Mamlaka ya usimamizi wa mfereji wa Suez ya Misri (SCA) imefanya sherehe ya kuadhimisha miaka 150 ya kufunguliwa kwa mfereji huo jimboni Ismailia, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

  Mkurugenzi wa mamlaka hiyo Bw. Osama Rabie amesema, katika siku za karibuni, mamlaka hiyo itaendelea kufanya mageuzi ya usimamizi na kuboresha huduma na matengenezo ya mfereji huo kupitia kuongeza nguzo zinazosaidia meli kutia nanga, kupanua eneo la kusubiria na kuongeza idadi ya meli za kuondoa tope.

  Bw. Rabie pia amesema, mamlaka hiyo inapanga kuimarisha ulinzi wa urithi wa kitamaduni wa mfereji huo. Makumbusho ya mfereji huo yaliyojengwa kwenye makao makuu ya zamani ya mamlaka hiyo, pia yanatarajia kufunguliwa mwaka kesho.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako