• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China aweka wazi msimamo wa China kuhusu suala la Hongkong

    (GMT+08:00) 2019-11-18 17:14:03

    Hivi karibuni rais Xi Jinping wa China aliposhiriki kwenye Mkutano wa 11 ya viongozi wa nchi za BRICS, alidhihirisha msimamo wa China kuhusu suala la Hongkong, akisisitiza kuwa, kipaumbele kwa Hongkong ni kusimamisha vurugu na kurejesha utaratibu. …….

    Serikali kuu ya China itaendelea kumuunga mkono kithabiti ofisa mkuu wa Hongkong kutekeleza majukumu kwa kufuata sheria, kuunga mkono kithabiti polisi ya Hongkong kutekeleza majukumu, na kuunga mkono kithabiti mamlaka ya sheria ya Hongkong kuwaadhibu wahalifu wanaotumia mabavu kwa kufuata sheria. Hatua hizo zimeonesha msimamo thabiti wa serikali kuu ya China wa kuunga mkono mamlaka ya mkoa wa utawala maalumu wa Hongkong kushughulikia suala la mkoa huo kwa kufuata sheria, na kudhihirisha upande wa utatuzi wa suala la mkoa huo.

    Katika miezi mitano iliyopita, wahalifu wanaotumia nguvu waliweka vizuizi barabarani, kufanya vurugu, unyang'anyaji, kuchoma moto, na kuwashambulia polisi. Madhumuni yao ni kuvuruga jamii ya Hongkong, kuteka serikali ya mkoa wa umaalumu wa Hongkong, na kukwamisha hatua ya China ya kujiendeleza, vitendo ambavyo vimevuruga usimamizi wa sheria na utaratibu wa jamii, kuharibu ustawi na utulivu wa Hongkong, na kutishia vibaya kanuni ya "China moja mifumo miwili", hatua ambayo haitavumiliwa na nchi na jamii yoyote. Kama rais Xi Jinping alivyoeleza, kipaumbele kwa mkoa wa Hongkong ni kusimamisha vurugu na kurejesha utaratibu.

    Polisi wa Hongkong, ikiwa nguvu muhimu ya kulinda usalama wa jamii mkoani humo, siku zote wako katika mstari wa mbele wa kupambana na wahalifu wanaotumia nguvu. Wanalinda utaratibu wa jamii kwa kuzuia vitendo vya watu wanaotumia nguvu kuwazingiria, kunyang'anya silaha na kutishia usalama wa jamaa zao. Lakini baadhi ya vyombo vya habari vya Hongkong na nchi za magharibi zinawapakia matope polisi hao kwa kuwashutumu kwa "matumizi mabaya ya nguvu", hali ambayo imeonesha vya kutosha vitendo vyao vyenye "vigezo viwili" na ukosefu wa maadili. Je, nchi gani za magharibi zinazokandamiza mara kwa mara maandamano kwa nguvu, kuweza kuonesha kiwango cha juu cha utekelezaji wa sheria na msimamo wa kujizuiza kama walivyofanya polisi wa Hongkong kwa kukabiliwa na vitendo vya kimabavu? Msimamo wa kiongozi wa China wa kuunga mkono kithabiti polisi wa Hongkong kutekeleza sheria, hakika ni tishio kubwa kwa wahalifu wanaotumia mabavu.

    Jambo linalofurahisha watu ni kwamba, wakazi wengi zaidi wanatembea barabarani kusafisha vizuizi barabarani, kuwaondoa watu wanaotumia nguvu na kuwatia moyo polisi kwa kujitolea kwao. Endapo watu wa hali mbalimbali wa mkoa wa Hongkong watatambua wazi sura halisi ya wahalifu wanaotumia nguvu, kuunga mkono kithabiti serikali ya mkoa huo, polisi na mamlaka za sheria kuwaadhibu wahalifu hao, hakika utaratibu wa kawaida wa Hongkong utarejeshwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako